SERIKALI YA AWAMU YA SITA RAHA TELE
Serikali ya awamu ya sita inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Changarawe kutoka Ibililo mpaka Kyosa kata ya Lupepo yenye umbali wa Km 10.
Barabara hiyo inayosimamia na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) awali inatarajiwa kujengwa umbali wa KM 04.
Mapema mwishoni mwa mwezi uliopita kamati ya siasa wilaya ya Rungwe inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu Mekson Mwakipunga ilizindua barabara hiyo na kuagiza ikamilike mapema kabla msimu wa mvua haujaanza.
Barabara hiyo ni muhimu na kiungo cha usafirishaji wa mazao ya kahawa, ndizi, mbao, Parachichi, maziwa na iliki kutoka kwa wakazi waishio katika miinuko ya kijiji cha Kyosa na vitongoji vyake .
Kwa sasa mara barabara hii itakapokamilika itarahisisha shughuli za uchukuzi, na kusaidia wagonjwa kuzifikia huduma za afya kwa urahisi zaidi.
Wakazi wa kijiji hiki wamefurahi barabara hii kuwafikia katika maeneo yao.
Alinanuswe Mwakalasya ameeleza kuwa kabla ya kujengwa walilazimika kubeba wagonjwa kwa kutumia machela kutoka eneo moja hadi lingine kufuata huduma ya afya.
Musa Kajoka anasonga mbele zaidi na kueleza kuwa kwa muda mrefu walanguzi wamekuwa wakishusha bei ya mazao ya shambani kwa kisingizio cha gharama ya usafirishaji lakini barabara hii inaenda kuondoa hiyo changamoto na hatimaye bei kupanda zaidi.
Tarura Tanzania
Ikulu Mawasiliano
Msemaji Mkuu wa Serikali
TANROADS
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa