Kupitia Ukurasa wa instagram wa shaderoom_tz ilichapishwa taarifa dhidi ya ya shule ya Msingi Mabonde iliyopo Kata ya Msasani.e
Moja ya mambo yaliyoandikwa ikiwa ni Malalamiko ni kuwa shule hii Wanafunzi wanachangishwa michango isivyostahili, Wanafunzi wa madarasa tofauti kuchanganywa chumba kimoja wakati wa masomo, Madaftari pamoja na Majibu yasiyo na staha kwa wazazi.
Ufuatao ni ufafanuzi dhidi ya Tuhuma hizi:
Kwanza ifahamike kuwa shule haiwezi kuanzisha mchango wowote kwa wanafunzi au Wazazi bila kikao na maridhiano ya wazazi. Kikao hicho ambacho husimamiwa na Mwenyekiti wa shule ndicho chenye Mamlaka dhidi ya Maendeleo na Ustawi wa shule katika eneo husika.
Mathalani tarehe 8/2/2022 Kikao cha Wazazi kikiongozwa na Mwenyekiti wa shule kiliazimia kuwa kila mzazi kuhakikisha anachangia chakula cha mchana kwa wanafunzi ili kuwaongezea lishe sambamba na kuongezea ufaulu katika shule hizi.
1. KUWACHANGANYA WANAFUNZI .
Wanafunzi wa darasa la III na la IV pia darasa la IV na vII hawachanywi pamoja wakati wa masomo. kwani Kila darasa lina mada zake lengwa na kufuata mtaala Kama ulivyoelekeza na WIZARA . Wanafunzi wa Darasa la sita wanasoma mada zao na la Saba mada zao vivyo hivyo .
2. MICHANGO;
Shule ya msingi Mabonde haina michango ya sh 7000 kwa wiki kama ilivyochapishwa katika ukurasa . Bali kuna Mchango ambao walikubaliana wazazi kwenye kikao tarehe 27/10/2023 ambayo ni sh 1000 kwa ajili ya mitihani siku ya Jumamosi hiyo ni kwa ajili ya kuchapisha mitihani na kuidulufu na Kila mtoto hupewa mitihani wake kwa ajili ya kutahiniwa.
3. MADAFTARI.
Kikao kilichokaliwa tarehe 27/10/2023 cha wazazi wa darasa la VI walikubaliana kwamba ; Kila mzazi atamnunulia mwanae MADAFTARI makubwa ili kuepuka usumbufu wa kununua MADAFTARI Mara kwa Mara hivyo wazazi wote kwa pamoja waliafiki na kuanza utekelezaji pia kutokana na walimu kukamilisha mada za darasa la sita mapema hivyo wameanza kuwafundisha wanafunzi mada za darasa la saba kuanzia tarehe 01/11/2023 ili kuwajengea uwezo mzuri kimasomo .Hakuna mwalimu yeyote aliyemfukuza mwanafunzi kwa kutoleta MADAFTARI MAKUBWA.
4. TUITION SHULENI.
Katika shule hii hakuna tuition yeyote inayoendelea SHULENI. Bali walimu wamejipanga kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wakati wa muda wa ziada kuanzia asubuhi na jioni ambayo ni bure.
5. MAJIBU KWA WAZAZI.
Katika shule hii uongozi wa shule hautoi majibu yasiyo na staha kwa Wazazi bali hutekeleza maazimio ya wazazi wenyewe ya kikao ambacho kilikaliwa tarehe 27/10/2023 ambacho wazazi walikubaliana kwamba mzazi ambaye atakuwa kinyume na maazimio ya kikao atachukuliwa hatua.
KWA HATUA HII: Tunaomba wazazi pamoja na wakazi wote wa Wilaya ya Rungwe kuepuka taarifa yoyote ya kupotosha ambayo inaweza kusababisha taharuki na hivyo kuondoa mshikamano na ufaulu wa wanafunzi wetu.
.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa