Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ipo mbioni kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Iponjola ambacho kinatarajia kugharimu kiasi cha shilingi MILLION 500 mpaka kumalizika kwakeFedha hizo zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita chini Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambapo kwa nchi nzima jumla ya vituo vya afya 70 vinajengwa kwa Ruzuku ya Serikali kuu kwa ghamara ya shilingi Billion 24.6kati ya hivyo vituo 70 vya afya Halmashauri ya Rungwe imenufaika na vituo viwili ambavyo ni Kyimo na Iponjola
Kwa upande wa vituo vya afya vinavyojengwa kwa fedha za tozo ya miamala ya simu Halmashauri ya Rungwe imepata kituo kimoja kilichopo katika kata ya Ndanto kwa gharama ya shilingi Million 500 na nchi nzima jumla ya vituo vya afya 234 vinajengwa kwa gharama ya shilingi Billion 117. kituo cha Ndato kipo katika hatua nzuri na majengo ya awali yanaanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya wahudumu walipangwa kuripoti.
Ujenzi wa majengo mengine unaendelea.
Kwa kutumia mapato ya ndani jumla ya vituo 103 vinajengwa nchi nzima kwa gharama ya shilingi Billion51.5 na Halmashauri ya Rungwe inajenga kituo hicho katika kata ya Kinyala kwa gharama ya zaidi ya shilingi Million 201.
Kwa upande wa ukamilishaji jumla ya maboma 763 yanakamilishwa ambapo zahanati 564 kwa kutumia ruzuku ya serikali yatakamilishwa kwa gharama ya shilingi Billion 28.2 nchi nzima, Mapato ya ndani zahanati 119 Billion 9.9
Majengo ya wagonjwa wa dharula 80 yanajengwa nchi nzima kwa shilingi Billion 24 na Hospitali ya Tukuyu imenufaika kwa mkoa mzima wa Mbeya kwa gharama ya Shillingi Million 300.
Kwa upande wa nyuma za watumishi jumla ya nyumba za watumishi wa afya 150 zinajegwa nchi nzima kwa gharama ya shilingi Billion 13.5 na Rungwe imenufaika kwa kituo cha afya Kyimo na zahanati ya Kyobo kata ya Iluti.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa