Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) imeendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwa binadamu katika maeneo tofauti wilayani Rungwe.
Katika kijiji cha Katabe kata ya Kyimo iliarifiwa kuwa sehemu kubwa ya wananchi wamekuwa wanatumia dawa bila kuzingatia masharti ikiwa ni pamoja muda wa matumizi hali inayochochea ongezeko la usugu wa magonjwa sambamba na kushusha uchumi wa nchi.
Aidha imesisitizwa kuwa watumiaji wa dawa wanatakiwa kusoma masharti na matumizi sahihi ya dawa hizo kabla ya kutumia ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza na hivyo kuathiri afya ya mwili.
Katika maeneo yote tofauti Watanzania wamekumbushwa kuendelea kupata chanjo dhidi ya COVID 19 ikiwa ni kinga madhubuti na sahihi na hivyo kuepukana na maambukizi ya virus vya CORONA.
Timu ya TMDA imetembelea shule ya Sekondari Lupoto, Bulyaga, Mpugugo, Iponjola pamoja na kijiji cha Katabe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa