====TMDA KAZINI===
Katika kuhakikisha wananchi wanajengewa uelewa namna ya kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa Wizara ya Afya kupitia TMDA kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu wameanza kampeni na elimu ya namna ya kutokomeza kadhia hii.
Katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe vijiji mbalimbali vimenufaika na mafunzo haya ikiwemo kyimo , Ndaga pamoja na
Goye.
Wananchi wamekumbushwa kuhakikisha wanashiriki kupima afya zao mara kwa mara sambamba na kupata dawa zilizosajiliwa na kuhakikiwa na Mamlaka kamili.
Imeelezwa kuwa kutumia dawa zisizo sajiliwa ni wazi itakuwa ngumu kutokomeza vimelea sugu vya magonjwa.
Aidha mara mgonjwa anapoona dawa anazotumia hazimletei mafanikio ameekezwa kuwaona watalamu wa afya pamoja na Mamlaka ya dawa na Vifaa tiba - TMDA.
Kampeni imeanza nchi nzima kuanzia Novemba 14 mwaka huu kwa kutoa elimu shuleni, vyuoni,sokoni, mikutano ya hadhara na maeneo mengine mengi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa