Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi.Loema I.Peter amefanya tathmini ya matokeo ya std Vii 2018. Tathmini hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri tarehe 8/11/2018,ilihudhuriwa na Walimu wa Wakuu wa shule za msingi zote wilayani Rungwe pamoja na Maafisa Elimu Kata wote.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa mwaka 2018 jumla ya shule za msingi zilizofanya mtihani wa darasa la saba ni 138 na shule zilizoongeza ufaulu ni 95 na shule 42 zimeshuka na sababu kuu za kushuka ufaulu huo ni usimamizi mbovu wa Walimu Wakuu hao na ndiyo sababu ya kuvuliwa nyadhifa zao.
Pia katika tathmini hiyo shule zilizofanya vizuri zilipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, pia amewataka Walimu Wakuu waliobaki katika nafasi za uongozi na Maafisa Elimu Kata kuandika barua za kuahidi kwamba watahakikisha ufaulu wa mwaka 2019 utapanda kwa 89% na kuahidi kama hawatofikia malengo watajihudhuru na barua hizo ziwe tayari tarehe 13/11/2018.
Aidha amemuagiza Afisa Elimu Wilaya na Maafisa Elimu wasaidizi wake katika idara ya Elimu nao kuandika barua za kuahidi kuongeza nguvu katika usimamizi wa kazi zao.
Picha juu za juu baadhi ya Walimu Wakuu wakiwa kwenye kikao cha tathmini ya matokeo ya std vii wilayani Rungwe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa