Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) umewaleta pamoja wawezeshaji 38 ngazi ya wilaya (kutoka Kata zote) ukilenga kutoa mafunzo elekezi juu ya kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kutoa ajira za muda katika maeneo mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi halmashauri ya wilaya Rungwe, Bi. Husna Tonni ambaye pia ni Afisa mipango wilaya , amewaomba wanufaika wa mafunzo hayo kwenda kuibua miradi Kwa weledi mkubwa huku wakilenga miradi inayotekelezeka na yenye hitaji halisi la jamii katika eneo husika.
Aidha afisa miradi TASAF makao makuu Eng. Thadei Shirima ameainisha baadhi ya miradi kuwa ni pamoja na elimu, afya, ustawi wa Jamii, kilimo, uvuvi, misitu, na ufugaji.
Katika ngazi ya utekelezaji wa miradi wanufaika watapata ujira Kwa kushiriki utekelezaji wa miradi yao ikiwa ni pamoja na ujuzi ambapo upacha huo utawasaidia kuondoa umasikini na kuwajengea maisha endelevu na yenye kipato chenye tija.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa