Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani leo tarehe 03.5.2023 umepitisha Rasimu ya Bajeti ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini (TARURA)yenye jumla ya Shilingi Billion 7.7 kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Bajeti hii itasaidia uborereshaji miundombinu ya barabara ikiwemo madaraja, ujenzi wa barabara mpya ,Ukarabati pamoja na ufungaji wa taa .
Bajeti hii inatokana na tozo ya mafuta ya dizeli na petroli inayokatwa kwa kila lita moja ya mtumiaji , Mfuko wa jimbo na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe.Mpokigwa Mwankuga ameishukuru TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya kuhakikisha Barabara za vijijini zinapitika na hivyo kuwezesha mazao ya wakulima kufika sokoni kwa urahisi.
Ameeleza kuwa licha ya Mvua kunyesha kwa wingi mfululizo katika wilaya ya Rungwe na hivyo kupelekea barabara kuharibika bado TARURA wamekuwa mstari wa Mbele kuzikarabati na kuzirudisha katika ubora wake.
Mhe. Mwankuga amezitaja moja ya barabara zilizojengwa kwa mwaka huu wa fedha kuwa ni pamoja na ile ya Masukulu -Kikole- Kipande(Kyela) na Kapugi- Lyenje na Masebe - Mpata(Busokelo).
Akiwasilisha bajeti hiyo, Meneja TARURA Wilaya ya Rungwe Mhandisi Derick Kamala amearifu kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali inatarajia kuweka tabaka jipya la lami katika barabara ya Mzunguko -TANESCO- TUKUYU Sekondari, Mzunguko -TRA na TANESCO -Bomani.
Aidha barabara ya Ibililo -Matweli pamoja na Ikuti- Mboyo itajengwa na hivyo kusaidia wakazi wengi wanaoishi katika maeneo hayo kufanya shughuli zao za kiuchumi, na kijamii kwa urahisi na haraka zaidi.
Rasimu huu ya Bajeti inaendelea kwa hatua zingine za utekelezaji.
Tarura Tanzania
Renatus Mchau
Ofisi ya Rais - Tamisemi
RUNGWE YETU" Mbeya".
Rungwe Updates
Rungwe Connection
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa