Zabuni ya ujenzi wa Soko la kisasa la ndizi Na.78J2/2024/2025/W/04 imerudiwa tena kutangazwa baada waombaji wa awali kukosa sifa.
Soko hili lililopo Karasha Kiwira kando ya Barabara kuu iendayo nchini Malawi ujenzi wake utakapokamilika utarahisha upatikanaji kwa urahisi wa ndizi kwa wafanyabiashara, bei nzuri kwa wakulima, Maegesho, Huduma za kifedha, Chakula na uhifadhi wa ndizi katika eneo lenye usalama wa kutosha (coldrooms).
Kwa taarifa hii watanzania wote mnahamasishwa kuomba tena zabuni ya ujenzi wa soko hili kupitia mfumo wa NesT kwa uchumi endelevu wa wilaya ya Rungwe na Tanzania kwa ujumla.
Ripoti ya:Noah Kibona
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri (W) Rungwe
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa