Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa wilayani Rungwe imearifu kuokoa kiasi cha TZS million 86,159,750.00 mali ya vyama vitano vya Ushirika fedha ambazo zingeliwa na watu wasiowaaminifu huku kiasi cha shilingi million 15,316,745.00 kikiwa tayari kimekabidhiwa kwa vyama hivyo mapema.
Kamanda wa taasisi hiyo wilayani Rungwe Bwana Mohamed Shariff amevitaja vyama hivyo kuwa ni ni pamoja na chama cha ushirika Kiwira SACCOS, KYIMO SACCOS, IKUTI SACCOS, ISEMPU AMCOS na AMANI MALANGALI.
Akikabidhi kwa wenyeviti wa vyama hivyo kiasi kilichobaki ambacho ni kiasi cha shilingi million 61,318,925.00 , Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe.Julius Chalya amewaomba watumishi wa vyama hivyo kuendelea kuwa waaminifu na waadilifu kwa kuhakikisha wanalinda mali za vyama hivyo kwa kuwakopesha wanufaika sahihi ili kuendelea kuwajengea uchumi endelevu na mhimili imara wa vyama hivyo.
Aidha amewakumbusha wanufaika kuhakikisha wanakopa kiasi cha fedha wanachoweza kumudu kukirejesha badala ya kukopa na kuziacha familia zao katika lindi la umasikini baada ya kushindwa kurejesha na kutumbukia katika mahangaiko huku vyama vya ushirika vikibaki katika hali ya kufilisika.
SOMA ENEO LA MATANGAZO KUONA JEDWALI LA MCHANGANUO WA FEDHA ZILIZOOKOLEWA
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa