Taarifa ya Utekelezaji wa ilani ya chama tawala (CCM) kwa miezi sita iliyopita imewasilishwa leo tarehe 20.08.2021 na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dkt. Vicent Anney.
Katika taarifa hiyo imeelezwa kuwa jumla ya shilingi Billion 2 zimetumika katika ujenzi wa barabara vijijini katika Halmashauri ya Rungwe, na Busokelo.
Aidha katika kipindi hicho Mradi wa umeme vijijini (REA) mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka jana jumla ya vijiji 70 kati ya 99 vimefanikiwa na kupata umeme huku juhudi zikiendelea kuhakikisha maeneo yote yaliyobaki yanapata nishati hiyo katika awamu hii.
Mhe. Anney amebainisha kuwa jumla ya lita million 60 za maziwa zinazalishwa katika wilaya ya Rungwe kwa mwaka lakini ukosefu wa viwanda na soko la uhakika linachangia bei ya maziwa kushuka. Katika kutafuta ufumbuzi, katika msimu huu jumla ya viwanda viwili vinatarajiwa kujengwa katika Halmashauri ya Rungwe na Busokelo vikilenga kuongeza thamani ya maziwa sambamba na upandishaji wa bei ambapo kwa sasa yanauzwa kwa wastani wa shilingi 650 kwa lita.
Hata hivyo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda vidogovidogo vya kuchakata mazao ya kilimo na mifugo katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hii ikilenga kuongeza thamani, ajira na soko la ushindani na hivyo kukuza wigo wa bei nzuri kwa mkulima.
Akizungumzia sekta ya utalii Dkt Anney ameongeza kuwa pamoja na kuwa na vivutio vingi katika wilaya hii lakini bado wananchi wameshindwa kuvitembelea mara kwa mara hatua inayoshusha pato la halmashauri na taifa kwa ujumla.
Pamoja na hayo sekta ya ulinzi na usalama, afya, maji, na elimu imeendelea kuboreka na kuimarika ambapo serikali inakikisha kila mtanzania anapata huduma bora na stahiki ili kuleta maendeleo yenye tija kwa kaya na taifa kwa ujumla.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa