UFAFANUZI DHIDI YA BANGO LA MEI MOSI
Siku ya wafanyakazi duniani maarufu kama mei mosi mwaka huu 2024 kulikuwa na Bango lililoandikwa "Walimu tumechoka na uhamisho usiokuwa na Malipo"
Tunaomba kukiri kuwa walimu wamekuwa na madai ya stahiki zao mbalimbali ambazo zimekuwepo katika vipindi tofauti.
Kuanzia mwaka 2014-2017 Serikali ilifanya zoezi la Kusawazisha Ikama ya walimu katika shule mbalimbali. Aidha Walimu waliokuwa wanafundisha masomo ya sanaa katika shule za sekondari sehemu yao walihamishiwa Shule za Msingi.Pia Walimu Wakuu waliokuwa na Elimu ya Cheti pia walishushwa Madaraka na kuhamishiwa katika shule mbalimbali huku Waliokuwa na Elimu ya Diploma na kuendelea wakachukua nafasi hizo.
Kutokana na hilo Deni la Madai ya Uhamisho lilifikia Shilingi Million 778,847,298.
Kupitia Mfumo wa Madenimis Serikali ilihakiki deni hilo na hivyo kuanza hatua mbalimbali za Malipo.
Serikali imeendelea kulipa madeni hayo kwa Walimu katika vipindi tofauti kila mwaka .
Barua yenye kumbukumbu namba RDC/CO/ED/T20/4/VOLII/161 Iitumwa Wizara ya fedha kwa ajili ya kukumbushia madai haya.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ndugu Renatus Mchau kwa kutambua mchango wa walimu katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi ameendelea kushughulikia madai haya kwa ukaribu sana.
Mwezi Marchi mwaka huu 2024 jumla ya shilingi million 12 zimelipwa kwa walimu katika shule mbalimbali ikiwa ni sehemu ya madai yao.
Pamoja na hayo jumla ya shilingi millioni 79 zinatarajiwa kulipwa kwa walimu wapatao 295 ndani ya mwezi huu Mei 2024.
Kwa sasa Mwalimu anapohamishwa analipwa mara moja stahiki zake zote kama Fedha za kujikimu na kusafirisha mizigo. Wastaafu pia wamekuwa wakisafirishiwa mizigo mara utumishi wao unapotamatika.
Hivyo tunapenda kuwashukuru walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya ambapo kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo ufaulu umekuwa kwa zaidi ya asilimia 94% na hivyo kushika nafasi ya pili kimkoa kati ya Halmashauri 07 zinazounda mkoa wa Mbeya.
Noah Kibona
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
09.5.2024
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa