Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kutumia Mapato yake ya ndani inaendelea na ukarabati wa stendi ya Mabasi Madogo iliyopo mkabala na Stendi kuu katika mji wa Tukuyu hatua itakayoboresha mazingira ya utoaji huduma ya usafiri kwa Wananchi.
Kwa mujibu wa Mpango wa Bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/ 24 , Stendi itakarabatiwa na kuwekewa " Tofali ngumu" ( Pavements blocks) na kufungwa taa hatua itakayorahisha shughuli ya usafirishaji na biashara kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe na Tanzania kwa ujumla.
Kwa mwaka huu pia stendi hii itawekewa jiwe la Msingi na Mbio za Mwenge siku ya tarehe 7.9.2023 ambapo Kimkoa utapokelewa katika kijiji cha Ikuti ukitokea Wilaya ya Ileje mkoani Songwe
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa