Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau anapenda kuwaarifu wakazi wote wa Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya na Tanzania Kwa ujumla kuwa soko la mbogamboga na Matunda lililopo Tandale Tukuyu Mjini limefunguliwa rasmi.
Soko hilo lililojengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri na Shirika la Agri- connect kupitia Mradi wa KIBOWAVI litawanufaisha zaidi ya ya wajasriamali 400 huku likiwa na vizimba 120 sambamba na Wafanyabiashara wengine watakao toa huduma kuzunguka soko hilo.
Aidha kumejengwa jengo maalumu la kukaushia na kuhifadhia mboga.
Kupitia kikao Cha kamati ya fedha, uongozi na Mipango kilichofanyika Leo tarehe 29.9.2022, Waheshimiwa Madiwani wameongeza ujenzi wa soko hilo na mazingira mazuri yalivyoboreshwa na kuishukuru Menejimenti ya Halmashauri pamoja na Wananchi kwa kusimamia vizuri ujenzi wa soko hilo.
Amenye Mwakatundu mkulima na Mfanyabiashara katika soko hilo ameishukuru Serikali kwa hatua nzuri iliyofikia na kuwa Sasa wataepukana na kadhia ya kunyeshewa na mvua pamoja na Mali zao Kukosa sehemu salama ya kufifadhia bidhaa zao.
Hata hivyo Wafanyabiashara katika soko hilo wamealika wateja wote katika viunga vya mji wa Tukuyu na Rungwe kwa ujumla kufika katika soko hilo na kujipatia mahitaji ya kila siku.
Soko la Tandale lipo katikati ya Gulio ambalo hufanyika kila siku ya Jumatatu na Alhamisi hali inayovutia Wafanyabiashara wengi kutoka katika wilaya ya Kyela, Busokelo, Chunya, Ileje, Mbeya, Njombe na Iringa kuja na kununua bidhaa za shambani zikiwa katika hali ya ubora.
Ndani ya soko hilo Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Rungwe Bwana Omary Mungu ameeleza Mpango pia ni kukarabati vyumba 40 vya Biashara na tayari 24 vimekamilika bado vyumba 16 ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa mitaro ya maji machafu na maeneo ya watembea kwa miguu.
"Katika kuhakikisha eneo hili linafikika kwa urahisi tunatarajia kuviondoa baadhi ya vibanda/ maduka Upande wa Barabara ya Tukuyu- Busokelo ili kutoa nafasi magari kushusha watu na mali zao kwa urahisi" ameongeza Bwana Mungi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa