Sogeza jiwe ni kampeni itumiwayo kuhamasisha ukarabati na ujenzi wa kituo cha afya Masukulu,ukarabati utafanyika kwa jengo moja la chumba cha kuhifadhia maiti na ujenzi wa majengo mapya ya chumba cha kuhifadhia maiti, chumba cha upasuaji, maabara,chumba cha kufulia,nyumba moja ya mtumishi,wodi ya wazazi,jengo la x rays na utrasound. Ujenzi huo umeanza mwezi huu wa tano na utakamilika mwezi wa tisa mwishoni. Ujenzi huo ukikamilika utasaidia jamii kupata huduma zote za afya ambazo kwasasa hazipatikani kituoni hapo na kuwafanya wagonjwa kusafiri umbali mrefu kwenda hospitali ya wilaya iliyoko Tukuyu mjini.
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ilipokea kiasi cha tsh 500,000,000.00 toka serikali kuu kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa kituo hicho cha afya. Ukarabati na ujenzi huo utafanyika kwa njia ya fosi akaunti Aidha kituo hiki kitakua kituo cha pili kupata pesa hiyo toka serikali kwaajili ya ukarabati na ujenzi ktuo cha kwanza kilikua ni Ikuti ambacho kwasasa ujenzi na ukarabati umefanyika.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mh.Ezekiel Mwakota aliwakabidhi wananchi mradi huo iliwaweze kushiriki katika ukarabati na ujenzi wa kituo hicho cha afya.
Mh.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe, akiwaongoza wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa kukabidhiwa mradi wa ukarabati na ujenzi wa kituo cha cha afya kwenda kusogeza jiwe kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa kituo hicho.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa