Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kiwilaya yamefanyika Leo tarehe 16.6.2021 katika shule ya msingi Ibililo iliyopo kata ya kata ya Nkunga.
Katibu tawala wilaya ya Rungwe bwana Mnkondo Bendera ndiye alikuwa mgeni rasmi ambapo ameagiza kila mzazi kuhakikisha analinda haki za watoto Kwa kutoa chakula shuleni, kutoa elimu stahiki Kwa watoto, kuwaepusha watoto na ndoa za utotoni hii ikiwa ni pamoja kuwaondolea vitendo vyote vya unyanyasaji
." Mitaala lazima iandaliwe ipasavyo ili maarifa wanayokosa nyumbani wayapate shuleni, na hii itawajengea uwezo mkubwa wa kupambana na mazingira yanayowazunguka" .
Ameongeza bwana Bendera.
Hata hivyo Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Rungwe bwana Omary Mungi amewakumbusha wazazi kuendelea kuzuia vitendo vyote vya ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na kuwapa mahitaji yote muhimu ya kibinadamu yakiwemo chakula chenye viini lishe na malazi bora.
Katika maadhimisho haya pamoja na elimu, burudani vilivyotolewa pia zawadi kadhaa zimetolewa Kwa wanafunzi waliofanya vizuri darasani huku Mgeni rasmi akiahidi kumnunulia sare za shule pamoja na mahitaji mengine muhimu Mwanafunzi Stain Lighton (ke) wa Shule ya Msingi Matweli anayesoma darasa la kwanza baada ya kushika nafasi ya kwanza Kwa misimu yote mfululizo.
Mwanafunzi huyo ambaye pia ana changamoto ya kutembea (mlemavu) ameshukuru msaada huo kwani utafungua ukurasa na safari yake rahisi ya kujipatia elimu.
Maadhimisho haya ni kumbukizi ya madhila waliyowapata watoto katika kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini mwaka 1976 na rasmi maadhimisho haya yalianza mwaka 1991 katika bara zima la Afrika
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa