Shule ya sekondari Wasichana Kayuki imeingia katika shule kumi bora za wananchi katika ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne 2021 nchini Tanzania.
Katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini shule nyingine ni Makete girls na hivyo kuwa na shule mbili tu za wananchi huku zingine zikitoka katika kanda zingine.
Shule hii ilifaulisha kwa daraja la kwanza wanafunzi 42, Daraja la pili wanafuzi 90, daraja la tatu wanafuzi 49, Daraja la nne wanafunzi 34 na sifuri mwanafunzi mmoja.Hali hii imesababisha Wizara- TAMISEMI kuikabidhi shule hii kikombe na cheti wiki iliyopita ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa shule hii katika utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wilayani Rungwe.
Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Bertha Sarufu ametaja sababu kadhaa zilizosaidia kupandisha ufaulu katika shule hiyo kuwa ni pamoja na Nidhamu nadhifu kwa wanafunzi, Walimu kujituma, kuwabaini wanafunzi wenye mahitaji ya ziada na kuwasaidia ipasavyo, kutoa motisha kwa kila mwanafuzi kwa kila mtihani nusu mhula na mwisho wa mhula, Bodi kutoa motisha kwa walimu waliofanya vizuri, kuondoa dhana ya masomo kuwa ni magumu kwa wanafunzi sambamba na kuwaita wanafunzi waliofaulu kuja kutoa ushuhuda kwa wenzao.
"Mathalani mwaka huu tumetoa motisha kwa wanananzi sita waliofaulu vizuri kwa kuwanunulia vifaa vya maandalizi ya kidato cha tano vyenye thamani ya shilingi 60,000/= kwa kila mmoja". ameongeza mwalimu Sarufu.
Shule hii inayopatikana katika kata ya Ilima hupokea wanafunzi wa kike kutoka katika shule zote za msingi wilayani Rungwe na hivvyo kuwa na tija kubwa kwa wakazi wote wa wilaya ya Rungwe.- Rungwe District Council-
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau amezitaja shule zingine zilizofanya vizuri kuwa ni pamoja na Tukuyu sekondari na Bulyaga na kuwa mikakati ni kuhakikisha shule zote zinafanya vizuri kwa walimu kufundisha kwa bidii, Uhakika wa chakula shuleni na utoaji wa motisha mbalimbali kwa walimu na wanafunzi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa