Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imetoa zaidi ya Shilingi million 700 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa majengo mapya na miundombinu ya Shule ya sekondari wavulana Rungwe.
Akizungumza katika hafla ya utambulisho wa mradi huo mbele ya wafanyanyakazi wa shule hiyo na serikali ya kujiji cha Ilolo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter amesisitiza mambo yafuatayo:
1.Fedha za serikali ni sumu, usifanyike ubadhilifu wa aina yeyote.
2.Manunuzi ya aina yeyote ile yafuate taratibu za serikali ni miongozo iliyotolewa.
3.Tunza nyaraka zote vizuri ili iwe rahisi kurejea kwa kila mtu na wakati wowote zikihitajika.
4.Msemaji wa taarifa ya ujenzi itolewe na mkuu wa shule kwa kushirikiana na kamati za ujenzi ili kuondoa mkanganyiko wa taarifa.
5.Watumishi wote mshirikiane na kufanya kazi kwa pamoja ili kuiletea heshima shule na taifa kwa ujumla.
6.Hakikisha mnapata mafundi wenye utashi na weledi wa kumaliza kazi haraka kwani mradi unatakiwa kukamilika ndani ya siku 90.
7 Hakikisha mnapata wazabuni wenye nia njema ya kuleta vifaa na kukamilisha mradi kwa wakati.
8. Majengo yatakayojengwa au kukarabatiwa lazima yalingane na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali.
9. Fedha zimetolewa kwa maelekezo hivyo miongozo izingatiwe na kufuatwa ili kuepuka mikanganyiko na kushindwa kukamilika kwa mradi.
10.Tusifanye maboresho yoyote ya mradi bila mawasiliano na ngazi ya juu kwani kushindwa kufanya hivyo itaongeza gharama ya mradi bila sababu.
Pamoja na mambo mengine ukarabati na ujenzi huu utajumuisha maeneo yafuatayo:
1. Ukarabati wa mabweni 7
2.Ukarabati wa vyoo 5
3.ujenzi wa bweni jipya la kulaza wanafunzi 80
4. ujenzi wa madarasa 3
5. ukarabati wa jiko na Bohari.
6. Ukarabati wa zahanati ya shule.
7.Ukarabati wa maabara.
8. Ukarabati wa madarasa yote ya kidato cha tano na sita.
9. Ukarabati wa myumba za waalimu
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa