Mkurugenzi MTENDAJI halmashauri ya Rungwe bibi Loema Peter amekabidhiwa kiasi cha TZS milioni 20 kutoka kwa Mkuu wa mkoa Mbeya Mhe. Albert Chalamila, ikiwa ni ahadi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli jana kwa wakazi wa kijiji cha Isyonje ambapo pamoja na mambo mengine ameruhusu wakazi wa kijiji hicho kuendelea kutumia eneo Lao ambapo awali lilikuwa litumiwe na TANROAD kwa ajili ya kujenga mizani.
Fedha hizo zitatumika kujenga madarasa mawili ya shule ya msingi Isyonje ambapo itajumuisha juhudi za halmashauri na nguvu kazi ya wananchi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa