Wakazi wa kitongoji cha Syukula na Kibisi mamlaka ya Mji mdogo Tukuyu halmashauri ya wilaya ya Rungwe wamehamasika na ujenzi wa shule mpya ya sekondari ikiwa ni jitihada ya kuwapunguzia watoto wao kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika maeneo ya jirani.
Shule hiyo iliyopo katika kitongoji cha Kibisi kilometa chache kutoka stendi ya Mwambegele (Kando ya mlima Rungwe) inatarajia kuwanufaisha wanafunzi wengi ambao awali walikuwa wanasoma katika shule ya sekondari Kyimo na Lupoto.
Aidha Mwenyekiti wa kitongoji hicho Bwana Baraka Mwakikuti amearifu kuwa kiwanda cha MAJI TUKUYU ( Tukuyu spring water) kimetoa jumla mabati 100 kama sehemu ya kurejesha huduma Kwa jamii ( Corporate social responsibility -CSR) huku Mbunge jimbo la Rungwe Mhe. Antony Mwantona akiahidi bati 100. Idadi hii itasaidia kumalizia hatua ya awali ya upauaji .
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa