SERIKALI YAZIDI KUPANUA HUDUMA YA ELIMU KWA WATU WAKE
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe baada ya kukamilisha ujenzi kwa kutumia Mapato yake ya ndani ipo mbioni kuanza kutoa huduma ya elimu katika shule mpya ya Msingi Umoja kwa Mchepuo wa Kingereza (Umoja English Medium).
Shule hii tayari imesajiliwa kwa namba EM.20613 na inapatikana katika eneo la Ilenge kata ya Kyimo barabara ya Sogea-Ipagika (Karibu na Shule ya msingi Ilenge.)
Shule nyingine ya Mchepuo wa Kingereza iliyosajiliwa na itaanza kutoa huduma ya elimu ni Ushirika English Medium inayopatikana Ushirika kata ya Mpuguso karibu na Shule ya Msingi Masebe.
Ushirika English Medium imesajiliwa kwa namba EM.20614
Hivyo Halmashauri ya Rungwe imekuwa na jumla ya shule tatu za mchepuo wa kiingereza ambazo ni Nuru, Umoja na Ushirika (Zinazomilikiwa na Serikali).
Pamoja na hizo Shule za Mchepuo wa Kingereza, Halmashauri imesajili na kufungua shule mpya kwa mchepuo wa kawaida katika kata ya IKUTI.
Shule hiyo ni shule ya Msingi Chief Mwanjali inayopatikana katika kitongoji cha Ipagika kijiji cha Ikuti.
Shule ya Msingi Chief Mwanjali imesajiliwa kwa namba 20615.
Hatua hii ya kufungua shule mpya isaidia kuongeza na kupanua maarifa na ujuzi kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe na taifa kwa ujumla.#kaziindelee
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa