Kifaa maalumu (Kishikwambi) kitatumika katika uhakiki na uboreshaji wa daftari la wapiga Julai mwaka huu 2024.
Kupitia mfumo wa Voters Registration System (VRS) Mnufaika atapata huduma bora kwa kasi na ufanisi mkubwa.
"Kura yako kwa Maendeleo ya taifa letu" Shiriki zoezi la uhakiki na uboreshaji wa daftari la wapiga kura ambalo linatarajia kuanza tarehe 1.7.2024 ambapo uzinduzi kitaifa utafanyika katika mkoa wa Kigoma.
Uboreshaji pia utajumuisha
✓uandikishaji wa Wapiga kura wapya ambao ni raia na wa Tanzania na wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakao timiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi Mkuu 2025
✓Wapiga kura waliopo kwenye daftari ambao wamehama kutoka eneo moja kwenda lingine
✓Kutoa fursa Wapiga kura waliojiandikisha kurekebisha taarifa zao kama majina na nyinginezo.
✓kutoa kadi mpya kwa walipoteza
✓kuondoa wapiga kura kwenye daftari kwa wale waliokosa sifa kwa sababu mbalimbali kama kifo, kuukana uraia wa Tanzania nakadhalika.
"KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA" Nenda kajiandikishe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa