SERIKALI YA MAMA SAMIA YAMWAGA BILLION 3 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO RUNGWE
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika hatua hii Imeumwaga Mwingi.
Halmashauri ya Rungwe imemwagiwa Mabilioni ya Fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
"Ama kweli hii ni serikali ya watu Chaguo la watu "
Billion 3 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miradi ya afya na elimu ambayo ndiyo nguzo mama ya maendeleo.
Serikali imetoa kiasi cha shilingi Billion 01 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje pamoja na wodi mbili za wagonjwa katika Hospitali ya wilaya " Makandana "
Vituo vipya vya afya vinaenda kujengwa katika kata ya Kiwira na Masoko ambapo kila kimoja kimepata shilingi Million 500.
Aidha vituo ambayo vimekamilika kama Iponjola, Ndanto Kinyala na Kalebela kila kimoja kimepata Million 150 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa tiba.
Pia Zahanati zilizokamilika kama Kyosa, ILENGE, Nkunga, Swaya zimepewa kiasi cha shilingi million 25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.
Zahanati ya Kyosa na Matwebe kila moja imekabidhiwa kitita cha shilingi million 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa majengo yake.
"Huyu ndiye mama Samia Suluhu Hassan "
Wakati huohuo nyumba mpya ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri inaenda kujengwa kwa shilingi gharama ya shilingi million 180 na fedha imepokelewa tayari.
Kwa upande wa Elimu Msingi Shule ya Msingi Katumba One imepata million 26.6 kwa ajili ya ujenzi wa darasa na vyoo, Shule ya msingi Bulyaga million 28.2 kwa ajili ya ujenzi wa darasa na vyoo pia.
Shule ya msingi Kigugu, Swaya, Mpunguti, Masebe, na Lupepo kila moja imepata donge nono la shilingi million 20 kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa.
Aidha Shule ya Msingi Mabonde na Iponjola kila moja imepata kiasi cha shilingi milioni 26.6 kwa ajili ya darasa na vyoo.
Million 30 zimetolewa na Mama Samia kwa ajili ujenzi wa Uzio katika shule yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu Katumba II
SEKONDARI:
Shule ya Sekondari kayuki imepokea kiasi cha shilingi millioni 41.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
Rungwe sekondari imepokea kiasi cha shilingi million 32.8 kwa ajili ujenzi wa chumba kimoja cha darasa na matundu 10 ya vyoo.
Isongole sekondari imepokea shilingi millioni 41.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
MPANGO WA SWASH
Kupitia mpango huu shule ya Msingi Bunyangomale, na Ibuka kila moja imejipatia shilingi million 41,214,815.02 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya vyoo.
FAIDA YA MIRADI HII
1.Itaongeza ajira kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe (Mafundi na Usambaji wa Chakula kwa mafundi)
2. Itaongeza mzunguko wa fedha katika Wilaya ya Rungwe
3.Itapanua upatikanaji wa huduma ya elimu na afya stahiki kwa wananchi
Renatus Mchau
Ikulu Mawasiliano
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Ikulu habari Zanzibar
CCM MKOA WA MBEYA
Msemaji Mkuu wa Serikali
RUNGWE YETU" Mbeya".
MBEYA YETU (GROUP LA MKOA WA MBEYA)
Wasafi TV
ITV Tanzania
Mwananchi
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa