SERIKALI YA AWAMU YA SITA YABORESHA MFUMO WA MANUNUZI
Mfumo mpya wa manunuzi kwa umma NeST ( National e-Procurement System of Tanzania) umewakutanisha watalamu kutoka Halmashauri saba zinazounda Mkoa wa Mbeya ukilenga kutoa Mafunzo na Matumizi Sahihi ya Mfumo huu
Mfumo huu ambao ni Mbadala wa ule wa awali wa TaNeps unaenda kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili watumiaji.
Faida ya Mfumo huu ni pamoja na kuondoa urasimu na matumizi sahihi ya muda , Hii ni kutokana na kila kitu kufanyika kwenye Mfumo ( Mtandao) na hivyo kuondoa matumizi ya karatasi na faili kuhama kutoka ofisi moja kwenda nyingine.
Ofisa wa Manunuzi anaweza kufanyia kazi maombi ya Manunuzi kutoka ofisi ya umma au Mzabuni popote alipo bila kuwepo ofisini na hivyo maombi kukamilishwa kwa wakati.
Mfumo huu umeunganishwa pia na mifumo mingine kama NIDA, Mapato, Fedha, Utumishi, Leseni na hivyo kutoa nafasi ya kupata taarifa sahihi za Mnufaika.
Mfumo huu Utakaotumika nchi nzima unatarajiwa kuanza kutumika rasmi tarehe 01.10.2023.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa