Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ipo mbioni kumaliza ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo katika kata ya Msasani mkabala na shule ya msingi Bulongwe.Shule hiyo yenye miundombinu yote ya kutolea elimu itakuwa na vyumba vya madarasa, maabara, chumba cha kompyuta, vyoo pamoja na jengo la utawala.
Mpaka kumalizika kwake ujenzi wa shule hiii utagharimu kiasi cha shilingi Million 600 na tayari serikali ya awamu ya sita imetoa shilingi million 470.
Miradi kama hii inaendelea katika maeneo mbalimbali ambapo kwa upande wa utoaji huduma ya afya kwa wananchi wake, Serikali imetoa kiasi cha shilingi million 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Iponjola, Million 500 kituo cha afya kata ya Ndanto,
Billion 1.3 katika hospitali ya wilaya Tukuyu, Million 150 zahanati ya Ilenge, Isyonje na Kyobo. Million 201 ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Kinyala kwa kutumia mapato ya ndani.Kuona miradi iliyotekelezwa katika robo ya tatu iliyopita fungua kiunganishi hiki: https://www.rungwedc.go.tz/.../6266842020e55716856169.pdf
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa