POCHI LA MAMA LAING'ARISHA NSONGOLA S/M.
Jumla ya shilingi million 25 ,000,000.00 zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Nsongola iliyopo kata ya Bujela.
Nyumba hii itaondoa changamoto ya makazi kwa walimu na hivyo kupanua wigo wa ufundishaji katika shule hii.
Wakazi wa kijiji cha Nsongola wameishukuru serikali kwa kuwaletea fedha hizo na kuahidi kuwa wataendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa kuibua na kukamilisha miradi Mbalimbali.
Asajile Mwangosi Mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa kabla ya ukamilishaji wa nyumba hiyo walianza kuijenga kabla ya mwaka 2016 ikiwa ni nguvu za wananchi na michango ya wadau.
Katika ujenzi huo walibahatika kujenga nyumba mbili za walimu lakini kwa hatua hii ya serikali kutoa million 25 kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba moja wanaishukuru sana.
Nje ya nyumba hiyo wakazi wa kijiji hicho wamejenga vyumba vinne vya madarasa na tayari vimeanza kutumika.
Juhudi zinazoendelea ni kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa nyumba zingine za walimu sambamba na kuendelea na zoezi la uchangiaji wa chakula shuleni ili kuongeza ufaulu.
Katika shule hiyo wanafunzi yenye wanafunzi 261 na walimu 06 wanapata chakula kwa asilimia 100%.
Ikulu Mawasiliano
Ikulu habari Zanzibar
Msemaji Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa