SERIKALI HII FURAHA YETU HAKIKA!!!
Hamna ubishi tena kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeupiga mwingi na kama ni matawi ni ya juu sana ni ngumu kuyafikia.
Tazama shule hii na miradi mingine katika picha imeota kama uyoga katika kata ya Lupepo ambapo ni sekondari Mpya kabisa katika kata hii na masomo tayari yanaendelea.
Shule kama hii pia imejengwa katika kata ya Msasani (Msasani one sekondari) na Kibumbe katika kata ya Kiwira.
Vituo vya afya Kyimo , Iponjola, Ndanto, Kinyala vimekamilika na Vile vya Masoko, Kiwira, Masebe, Malindo na Swaya ujenzi unaendelea.
Tabasamu mwanana linaendelea kutolewa na Wakazi wa Ndulilo -Itete kata ya Lufingo ambapo barabara kwa kiwango cha Lami inaendelea Kujengwa umbali wa Km 11 hii ni pamoja na usimikaji wa taa za barabarani.
Furaha itazidi kuongezeka mara baada ya kukamilika mradi wa maji Mbaka- -Tukuyu Mjini ambapo ujenzi unaendelea (Ujenzi wa tanki Msasani) na baadhi ya maeneo wanaendelea kupata maji kupitia mradi huu. Miradi mingine ni pamoja na Mradi wa maji Ikuti-Lyenje, Igalamo, Swaya. Masoko Group na Mradi wa maji Isaka kata ya Nkunga .
Baada ya serikali kutoa pikipiki kwa watalamu wa kilimo , Wakulima wanaopata huduma ya ughani imeongezeka kutoka wakulima 66,387 mwaka 2020 mpaka kufikia 70,105 Aprili 2023.
Uwiano wa wakulima wanaotumia mbolea ya Viwandani umeongezeka kutoka 76% mwaka 2020 mpaka kufikia 81% mwaka 2023
Kutokana na serikali kutoa Ruzuku katika Mbolea Mathalani Uzalishaji wa ndizi umepanda kutoka tani 352,848 mwaka 2020 hadi tani 356,404 mwaka 2022.
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Ikulu Mawasiliano
Msemaji Mkuu wa Serikali
Renatus Mchau
RUNGWE YETU" Mbeya".
MBEYA YETU (GROUP LA MKOA WA MBEYA)
Atubonekisye Mshani
Mbeya Press Club
MBEYA YETU WOTE
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa