Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa kushirikiana na kampuni ya ununuzi wa zao la kakao-Bioland imeendelea na ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali katika kata ya Kisiba, na Matwebe Tarafa ya Pakati na hivyo kuimarisha methali ya Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
Kampuni ya Bioland inafanya hivyo ikiwa ni rejesho kwa jamii ( Corporate social Responsibility-CSR) baada ya wakulima kuzalisha zao hilo kwa tija na kuiuzia kampuni hiyo.
Vyumba hivyo vilivyo katika hali ya ubora sana litakuwa suluhisho la msongamano wa wanafunzi darasani na mahali salama na sahihi pa kusomea na kujifunzia.
Mradi huu ambao umeanza kutekelezwa kwa miaka ya hivi karibuni ni endelevu na utazinufaisha shule nyingi.Katika kata ya Kisiba shule ya Msingi, Ikomelo, Masoko, Mbaka na Busilya zimenufaika na mradi huu.
Amani Mwafula mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Busilya ameshuhudia mabadiliko ya shule yao kwani kwa sasa wanakaa kwa nafasi, hewa nzuri darasani na tatizo la kukaa chini limemalizika.
Gwantwa Mwandambo mkulima wa zao la kakao na mkazi wa kijiji cha Lwifwa anaishukuru serikali kwa kuanzisha ushirikiano huo na kuwa sasa shule ya kijiji chao ina majengo mazuri na toka uhuru hawakuwahi kupata mradi mzuri kama huo.
Nae Joshua Mwakatumbula kiongozi wa mila na mkazi wa kijiji cha Mbaka anaona mbele zaidi na kubainisha kuwa kata hii imefunguka kwa kuwa na miundombinu bora ya elimu kazi kubwa iliyobaki ni walimu na wazazi kuitunza.
KAZI YA WALIMU
Uongozi wa shule pamoja na walimu wanajukumu la kudhibiti nidhamu ya wanafunzi dhidi ya kuchafua majengo na kuharibu samani.Jukumu lingine ni kuandaa masomo na kufundisha kwa mujibu wa mtaala wa elimu kwa lengo la kukuza na kendeleza maarifa na ujuzi ili kuongeza ufaulu. Hii itaonesha thamani ya majengo na uwekezaji uliowekezwa.
JUKUMU LA WAZAZI
.Kuratibu nidhamu ya watoto wao..
Kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi ili kuimarisha lishe.
Kushiriki shughuli za maendeleo ya shule
JUKUMU LA WANAFUNZI.
Kusoma kwa makini na kufaulu mbinu za mitihani zilizofumbwa..
Kutunza miundombinu ya shule na samani.
Kudumisha nidhamu shuleni.Kushiriki shughuli za uzalishaji mali shuleni (E.K)
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa