Taasisi isiyo ya kiserikali ya Rungwe yetu imetoa jumla ya mifuko 50 ya saruji Kwa halmashauri ya wilaya ya Rungwe ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za wananchi katika ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa Kwa ajili ya kidato cha kwanza mapema januari mwakani.
Akikabidhi stakabadhi ya malipo ya saruji hiyo, Mwenyekiti wa Rungwe yetu bwana Geoffrey Mwambene amesema kuwa msaada huo umetolewa Kwa lengo la kuboresha miundombinu ya ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuinua kiwango cha ufaulu Kwa shule zote wilayani Rungwe.
Hata hivyo akipokea stakabadhi hiyo, Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bi. Loema Peter amesema kuwa msaada huo umefika katika kipindi mwafaka kwani bado mahitaji na juhudi zinahitajika kukamilisha ujenzi wa madarasa Kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaanza masomo yao mapema mwakani.
"Msaada huu umefika katika mikono salama na niwahakikishie itafanya kazi iliyokusudiwa" amesisitiza.
Rungwe yetu pia imetoa mifuko 20 ya saruji Kwa halmashauri ya Busokelo.
BAADHI YA SHUGHULI ZILIZO FANYWA NA RUNGWE YETU:
1. Ugawaji wa Taulo za kike mashuleni
2.Uhamashaji KILIMO cha kahawa na parachichi Kwa wananchi
3.Ushiriki ujenzi wa choo hospitali ya wilaya Tukuyu-MAKANDANA4.Utoaji wa misaada Kwa watu kwenye mahitaji maalumu mfano Shule ya msingi KATUMBA Mchanganyiko.
5. Uhamasishaji wa wadau mbalimbali kuwekeza katika wilaya ya Rungwe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa