Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango kikubwa katika wilaya ya Rungwe.
Katika hatua hii barabara ya Tukuyu- Busokelo ipo mbioni kukamilika baada ya kipande cha Km 7 kuwa katika hatua ya ukamilishaji kutoka Tukuyu Mjini.
Barabara kutoka Lwangwa (Busokelo) mpaka Mbambo-Mto Mbaka imefikia kiwango kizuri cha ujenzi wake.
Haya ni mafanikio makubwa kwa Serikali kuhakikisha watu na mali zao wanasafirisha kwa haraka na ufanisi mkubwa.
Baada ya barabara hii kukamilika ; ni wazi gharama ya usafirishaji itapungua hususani kwa wagonjwa kufuata huduma ya matibabu katika hospitali ya Rufaa na Kanda Jijini Mbeya.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa