Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imeshiriki Leo tarehe 09.11.2022 katika Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yanayoendelea katika eneo la Kihesa Kilolo Manispaa ya Iringa.
Mhe. Dkt. Pindi Chana Waziri wa Maliasili na Utalii ndiye alikuwa Mgeni Rasmi na ameyafungua Maonesho hayo mapema Leo Mchana.
Akizungumza na Wadau wa Utalii waliojitokeza kwa wingi Mhe. Chana amewakumbusha Watanzania kuwa fursa za uwekezaji zipo nyingi katika sekta ya utalii na kuwa kufanya hivyo itachochea ukuaji wa uchumi nchini.
Dk Chana amepongeza Filamu ya The Royal Tour iliyoasisiwa na kuendeshwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kama Mhusika Mkuu kuwa imeongeza idadi ya Watalii nchini mpaka kufikia watu Million 1.34 tofauti na hapo kabla kitecho kilichosaidia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Aidha Dk Chana ameonya tabia ya Watanzania kuharibu uoto wa asili kwa kuchoma moto na kukata miti hovyo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira na matokeo yake ni ukame wa kudumu, mmomonyoko wa ardhi na ukosefu wa maji.
Katika Maonesho hayo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe Dkt Vicent Anney kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameutaja Mti Katembo uliopo kata ya Kisiba kuwa ndiyo Mti mnene zaidi Tanzania na kuwa ili kuunzunguka unahitaji watu wazima 12 walioshikana mikono kwa kuzunguka.
Karibu UWEKEZE katika vivutio Wilayani Rungwe eneo ambalo kila kipande kinafaa kuwekeza mtaji wako kwa faida lukuki.
Kwa gharama ya Kawaida kila Mtanzania anaweza kutembelea vivutio vyetu RUNGWE. Mtu mzima ni shilingi 2000 chini ya miaka 18 ni shilingi 1000 chini ya miaka mitano ni Bure. Watalii toka nje ya nchi ni Dola $5.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa