Kuelekea miaka miwili tangu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM)Taifa kimefanya ziara katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe na kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho tawala nchini.
Bi.Happynes Sule Katibu Msaidizi Mkuu idara ya Itikadi na Uenezi Taifa ndiye aliyeongoza timu hiyo na kujionea namna miradi hiyo ilivyotekelezwa kwa kishindo.
Akiwa katika jengo la wagonjwa wa dharura -EMD hospitali ya wilaya Tukuyu maarufu kama Makandana Bi. Sule ameshukuru kwa hatua ya ujenzi wa jengo hilo iliyofikiwa na kuwa wananchi waendelee kuiunga serikali kwa miradi mingine inayoendelea kwa kuchangia nguvu zao sambamba na kuitunza ili idumu kwa muda mrefu.
Amesema serikali imetoa kiasi cha shilingi million 300 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo hali itakayoongeza ufanisi na uhakika wa matibabu kwa wagonjwa.
Aidha amewaagiza watumishi katika hospitali hiyo kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yao ili thamani ya fedha iliyotolewa na serikali ilingane na kiwango cha huduma kinachotolewa kwa wagonjwa.
Katika hatua nyingine Bi.Sule amepongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Baraza la Madiwani, Menejimenti, Watumishi pamoja na wakazi wote wa wilaya ya Rungwe kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo sambamba na utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi -CCM
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa