ELIMU YA WATU WAZIMA YAZIDI KUPANUKA RUNGWE
Halmashauri ya Rungwe imeendelea kuboresha mazingira mazuri kwa kutoa elimu bora dhidi ya watu wazima ambao kutokana na sababu mbalimbali hawakupata elimu katika mfumo rasmi.
Elimu ya watu wazima ni mfumo wa utoaji elimu kupitia Kisomo chenye manufaa, Kisomo Cha kujiendeleza, MEMKWA, Shule huria, vituo vya ufundi- stadi, Mpango wa uwiano kati ya jamii na elimu ya watu wazima (MUKEJA) na taarifa ya lishe na Chanjo shuleni.
Kupitia MUKEJA jumla ya wanafunzi 461 wanaendelea na Masomo katika vituo mbalimbali ambapo hujifunza maarifa na ujuzi katika shule za Msingi na Sekondari ambapo wametengewa madarasa maalumu ambapo hufundishwa baada ya muda wa kawaida.
Baadhi ya Mafunzo ni pamoja kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), mafunzo ya kilimo bora, ufugaji wa wanyama na samaki pamoja na ujasiriamali.
Shule zinazofundisha ni pamoja na Kanyegele, Iponjola, Lyenje, Ikuti, Bulongwe na zingine shule 33
Mwalimu Thomas Mwanga ni Afisa Elimu ya Watu wazima katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na ametaja baadhi ya mafanikio ya Mpango huu kuwa ni pamoja na kudahili wanafunzi wa kike 39 katika shule ya Sekondari Kiwira ambao walikatisha Masomo kutokana na sababu mbalimbali na Sasa wanaendelea na Masomo katika shule hiyo.
Mwanga ameeleza kuwa katika kituo cha Kanyegele licha ya kujifunza Masomo ya darasani wanafunzi wameanza kulima viazi mviringo ikiwa ni elimu kupitia Mpango wa MUKEJA wanayopewa darasani huku Syukula wakifuga samaki na Iponjola wakipanda zao la parachichi.
Kupitia elimu ya watu wazima jumla ya wanafunzi 33 wananufaika na elimu ya MEMKWA, 276 Elimu Masafa, 172 Shule huria, na 577 vyuo vya ufundi-.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa