RUNGWE SEHEMU YA PEKEE DUNIANI
Noah Kibona PR-IO , RUNGWE DC
Utalii wa ndani unaanza na mimi na wewe.
Ukiwa Kijiji cha Ntandabala (Pakati) kata ya Masoko unapata kujikumbusha na mambo mengi ya kale.
Jengo linaonekana hapo limebeba historia maarufu wilayani Rungwe na Mkoa wote wa Mbeya,Hapa panaitwa Council au Pakati ikiwa na maana sehemu ya katikati.
Mzee Thabiti Mwapagata ni mzaliwa na mwenyeji wa kijiji hiki.
Mzee huyu alizaliwa mwaka 1930 na alishuhudia wakati jengo hili linajengwa.Jengo hili lililojengwa mwaka 1951 kwa amri ya Malikia wa Uingereza lililenga kuwa makao makuu ya utawala wa kikoloni hasa likitumika kama Halmashauri ya Machifu 12 kutoka wilaya ya Kyela, Ileje, Mbozi, Mbeya, Busokelo na Rungwe yenyewe.
Sehemu hii ilitumika kwa ajili ya mashauri na kesi mbalimbali zilizokusanywa maeneo mbalimbali.Mzee Mwapagata anasema jengo hili lilifunguliwa mwaka 1953 na Chief Adam Sappi Mkwawa kutoka Iringa kwa amri ya Gavana wa Tanganyika wakati huo.
Mwapagata anaeleza kuwa Adam Sappi alikuja kulifungua kutokana na machifu wakati huo kutoka Mbeya kushindwa kuafikiana namna bora ya kulifungua.Ndani ya jengo hilo kulikuwa na Kasiki (safe- strongroom) kwa ajili ya kutunzia mishahara ya wafanyakazi kutoka wilaya zote
Kasiki hii bado ipo na watu kadhaa wamejaribu kuivunja na kutaka kubaini kama ndani yake kuna masalia ya fedha na wameshindwa bila mafanikio yeyote.
Kilometa chache kutoka hapa Masoko (Pakati) kulijengwa ngome ya kijeshi wakati wa ukoloni katika kijiji cha Lwifwa kata Kisiba.Ngome hii ipo kando ya ziwa Kisiba na ilitumika na wakoloni kama kituo cha kulinda usalama katika kanda hii.
Majengo hayo mpaka leo yapo na yamejengwa kwa mawe.Kutokana na sababu mbalimbali Ngome hii ilihamishiwa Tukuyu Mjini ambapo sasa ni makao makuu ya Wilaya ya Rungwe.Na hapa ilikuwa rahisi kutawala na kuyafikia maeneo yote Mkoa wa Mbeya.Majengo mengine kama hili (Pakati) lipo Kyimo kata ya Kyimo na Busokelo.
Jengo la Kyimo sasa limekarabatiwa na ni makao makuu ya TARAFA ya Ukukwe. Jengo la Pakati limebaki urithi wa kihistoria huku ofisi ya tarafa ikijengwa kando yake.
Majengo mengine ya kihistoria ni pamoja na Kanisa na majengo ya washukiwa wa Ukoma Kisa kata ya Kisondela, Rungwe mission, majengo ya utawala Rungwe makao makuu, na mengine mengi.
Vivutio vingine ni Mlima Rungwe wenye urefu zaidi Nyanda za juu kusini, ziwa Ngosi na Kisiba, Maporomoko ya maji Kaporogwe, Mwandambo, Isabula, Malamba, kapiki na Malasusa.
Kuburi kubwa zaidi wilaya ya Rungwe la chifu Mwakatumbula, Mti mkubwa zaidi nchini Tanzania ( mti katembo) ,pamoja na Utalii wa mazao kama Chai, kahawa, kokoa, vanilla, na Parachichi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa