Noah Kibona, Rungwe DC
:Takribani Km 14 kutoka Tukuyu mjini barabara ya Busokelo unakutana na makao makuu ya kata ya Kisiba Boma la zamani la utawala wa serikali ya ukoloni wa Kijerumani kabla ya kuhamia Tukuyu na mpaka sasa majengo yapo.
Mto Mbaka ndio mpaka wa Halmashauri ya Busokelo na Rungwe ambao unakadiliwa kuwa na urefu wa Km 100 kutoka chanzo chake mlima Rungwe kuelekea ziwa Nyasa.
Kando ya mto huu mita kadhaa juu ya kivuko cha KIBUNDUGULU (kiteputepu) kuna chemichemi ya maji ILWALILO.ILWALILO kwa lugha ya wenyeji "Wanyakyusa" humanisha eneo la kupata matibabu.
Simulizi za wakazi wa eneo hili kijiji cha Lwifwa (Isesero) wanataja kuwa awali kabla na baada ya ukoloni eneo hili lilitumiwa kuondolea mikosi na magonjwa ya ngozi kama upele, ukoma na mengine mengi.
Chemichemi hii iliyojitokeza katika uoto wa asili ina maji ya moto masaa 24 na wenyeji huyatumia kwa shughuli za kitabibu na kuogelea kama sehemu ya burudani hasa kutokana na kuwa na maji ya moto na uvuguvugu pale yanapokutana na mkondo wa maji baridi.
Safari ya kufika eneo hili inakuleta kwa kupitia kivuko cha kibundugulu au kupitia shule ya msingi Masoko, - mti katembo- Shule ya msingi Isesero mpaka maji maji moto Ilwalilo.
Viuvutio vingine vilivyopo katika kata hii ni pamoja na ziwa kisiba, Mti mnene zaidi Nyanda za juu kusini - Katembo, Maporomoko ya maji Mwandambo, Maporomoko ya maji Isabula, Kaburi na boma la Chifu tajiri zaidi Wilaya ya Rungwe wakati wa ukoloni-Mwakatumbula, Boma la Wajerumani na Utamaduni wa kabila la Kinyakyusa.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa