CHANJO YA POLIO NYUMBA KWA NYUMBA
Kikao cha Kamati ya afya ya Msingi kimeketi leo tarehe Maudhui yakilenga katika kampeni dhidi ya ugonjwa wa POLIO.
Kikao kimeongozwa na Katibu tawala Wilaya ya Rungwe Bwana Ally Kiumwa ambapo amesisitiza wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, elimu, wazazi, vyombo vya habari, pamoja taasisi anuai kuhakikisha zinajitokeza kifua mbele kutoa elimu, kuibua na kuwapeleka watoto kupata chanjo.
Ugonjwa wa POLIO ambao kwa mara ya Mwisho Tanzania ilipata Mgonjwa wake mwaka 1996 hivi karibuni katika hatua nyingine Mgonjwa amegundulika Sumbawanga Mkoani Rukwa
Hatua hii mefanya Serikali kufanya kampeni na chanjo katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Katavi, Kigoma na Kagera.
Walengwa ni watoto walio chini ya miaka 8 watakaopatikana katika shule za Msingi, Nyumbani, Vituo vya kulelea watoto, na shule za awali,
Zoezi litadumu kwa siku nne kuanzia tarehe 21-24 septemba 2023
POLIO NINI?
POLIO ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya polio
Ugonjwa huu humsababishia Mgonjwa kupooza viungo vya mwili na hatimaye kifo
Virusi vinaweza kuingia kwa njia ya mdomo kwa kunywa maji au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa na virusi hivyo
POLIO haina tiba lakini inaweza kuzuiliwa kwa kupata chanjo ya polio ya matone au sindano (IPV).
Ikumbukwe kuwa chanjo ya Polio haina madhara yoyote. Mtoto anaweza kupata chanjo ya polio mara nne au zaidi ili kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa huu.
Mganga Mkuu wilaya ya Rungwe Dkt.Diocles Ngaiza ameeleza kuwa Chanjo pamoja na vifaa vyake vimesambazwa katika kata zote 29 zinazounda Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ambapo vijiji vyote 99 vitafikiwa.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa