" Wakazi wa Wilaya ya Rungwe tuache kuchanganya maji na maziwa tunayaondolea ubora na tunashindwa kuaminika na wawekezaji katika sekta maziwa"
Maneno hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Dkt. Vicent Anney wakati wa hafla maalumu ya kuhitimisha Mradi wa Tanzania Milk Processing Project (TMPP) Kanda ya nyanda za juu kusini.
TMPP iliyochini ya Heifer International imedumu katika wilaya ya Rungwe kwa muda wa miaka miwili.
Dkt. Anney ameshukuru Mradi wa TMPP kwa kazi kubwa ulioifanya katika kuboresha na kuongeza uzalishaji wa maziwa, kuongeza usawa wa kijinsia katika ufugaji na uzalishaji wa maziwa mpaka kufikia asilimia 40%, Ujenzi wa matanki ya kukusanyia maziwa na keni za kubebea maziwa, Gari la kukusanyia maziwa, na ugawaji wa Ng'ombe bora na elimu ya ugani kwa wafugaji.
Aidha ameishukuru kampuni ya ASAS Dairies kwa kuendelea kukusanya maziwa kwa wingi kupitia AMCOS mbalimbali na mfugaji mmoja mmoja na kuaigiza kampuni hiyo kuendelea kuboresha Bei ya maziwa kwa Lita ili kuongeza tija na maendeleo kwa dhahabu hiyo nyeupe Wilayani Rungwe.
Kampuni ya ASAS tayari imefikisha mitambo ya kusindika maziwa katika kiwanda chake kilichopo Kijiji Cha Ilenge kata ya Kyimo na itaanza kufungwa mapema Mwezi huu.
Zaidi ya asilimia 40% ya maziwa yanayosindikwa kupitia kampuni ya ASAS- Iringa huzalishwa Wilayani Rungwe kupitia wafugaji waliowezeshwa na Heifer International kupitia Mradi wa TMPP.
Wakati huohuo Dkt. Anney ameagiza wakazi wote Wilayani Rungwe kuhakikisha wanaboresha lishe kwa familia kwa kuhakikisha wanapatiwa maziwa kila siku na hivyo kuondokana na utapiamlo na udumavu hasa kwa watoto.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa