Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga (wa pili kulia) leo tarehe 29/10/2021 ameriarifu Baraza la Madiwani kuwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 kuanzia mwezi julai hadi septemba, Halmashauri imekusanya jumla ya shilingi 1,620,952,807.71 sawa na asilimia 122% ya makisio ya shilingi 1,326,564,689.00 kwa kipindi hicho cha julai hadi septemba 2021.
Aidha imeelezwa kuwa mapato hayo ni sawa na asilimia 31 ya makisio ya mwaka wa fedha 2021/22 yenye jumla ya shilingi 5,306,258,756.00
Makusanyo hayo yametokana na ushuru wa mazao, ada na ushuru mbalimbali, leseni anuai, mapato kutokana na mali za halmashauri, ushuru kutokana na mali asili, mapato kutokana na hisa, ICHF adaza shule na huduma za afya.
Mapato hayo yamekuwa chachu ya maendeleo kwa kujenga kituo cha afya kata ya Kinyala, Uboreshaji stendi ya mabasi, ukamilishaji wa zahanati ya Swaya, Marejesho ya asilimia 20% ngazi ya kata, Asilimia kumi 10% kwa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ununuzi wa pikipiki 04 za watendaji wa kata pamoja na ujenzi wa vyumba 05 vya madarasa.
Katika kufikia hatua hiyo ya makusanyo, Baraza la madiwani limemsifu Mweka hazina Wilaya Bwana Lucas Ndombele kwa kuwa chachu ya ukusanyaji wa mapato na kuwa hatua hiyo itaenda kuboresha huduma za kijamii sambamba na kuboresha maisha ya wakazi wa wilaya ya Rungwe.
Katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera, ambapo ameshauri fedha inayokopeshwa kwa vikundi kutotewa kwa vikundi vinavyoonesha nia ya kuanzisha viwanda na kuajiri watu wengi zaidi badala ya kutoa fedha kwa vikundi vingi visivyoonesha manufaa kwa jamii.
Mhe. Homera amevitaja viwanda hivyo kuwa ni pamoja na kiwanda cha Maziwa, biskuti, chokolate, njiti za meno na kadhalika.
Ametaja kuwa zaidi ya shilingi billion 3 zimeletwa katika wilaya ya Rungwe kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo waheshimiwa Madiwani washirikiane na wananchi pamoja na watalaamu ipasavyo kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
"Mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe! kutokana na makato ya miamala ya simu inayofanyika ndani ya wiki hii Serikali imetoa kiasi cha shilingi million 250 kwa ajili ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Ndanto. Piga makofi kwa Mama Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan" Amesisitiza.
Pia amearifu kuwa chuo cha Ualimu Tukuyu kimepokea kiasi cha shilingi million 500 kwa ajili ya ukarabati wa chuo hicho.
Pamoja na hayo Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vicent Anney ameonya kwa wale wanaolenga kuhujumu fedha hizo kuwa kwa kufanya hivyo watapunguza kasi ya ukamilishaji wa miradi na kuwaondolea wananchi huduma wanayotarajia kuipata baada ya Serikali ya awamu ya sita kuwapatia msaada huo.
Katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Rungwe Bwana Renatus Mchau ametaja kuwa ameandaa timu kambambe kila tarafa itakayofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kazi ya ujenzi inamalizika kwa wakati.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa