Mbele ya Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani leo tarehe 29/09/2021 Mweka Hazina Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bw. Lucas Ndombele amearifu kuwa kwa mwaka fedha 2021/2021 Halmashauri imeweza kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kukusanya jumla ya shilingi za kitanzania Billion 5,253,153,343 kati ya lengo la Shilingi Billion 5,371119,322 sawa na asilimia 99.Kati ya hizo fedha Shilingi Billion 2,015,117,330 zilitokana na mapato fungwa (CHF, papo kwa papo, NIHF na ada za shule) huku shilingi Billion 3,238,036,013 zikitokana na vyanzo mbalimbali vya Halmashauri.
Mapato hayo yameiwezesha Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kuongeza mali za kudumu kama majengo, gari na pikipiki, mitambo na mashine, samani na vifaa, vitabu, kompyuta na nyingine nyingi yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 4 kwa mwaka wa fedha 2020/21.
Moja ya majengo ni pamoja shule ya msingi Isyonje na Isuga, kituo cha afya Mpuguso, Ujenzi wa ofisi ya kata kiwira pamoja na stendi ya madukani, Ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Nkunga na Nuru Eng. Medium, Ujenzi wa kitega uchumi stendi ya mabasi, ujenzi wa soko la Mwambenja, Ukarabati chumba cha maiti- kituo ch afya Masukulu, Ukarabati jengo la mama na mtoto -Makandana, ukarabati wa nyumba za watumishi na mengine mengi.
Katika Mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ambaye pia ni Afisa utumishi wilaya Bwana Polycarp Ntapanya amearifu kuwa ifikapo kesho tarehe 30/9/2021 stendi ya daladala iliyopo Tukuyu mjini itaanza kufanyiwa ukarabati mkubwa ili kuwezesha wanufaika kuanza kuitumia katika hali ya unadhifu.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Vicent Anney ameagiza watu wote kuacha kutorosha mapato ili kuijengea uwezo serikali kuwaletea maendeleo endelevu na hivyo kutoa huduma stahiki kwa watu wake.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa