Kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kutoa mkopo wenye thamani ya Shilingi million 266 kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu hapo jana, Kikundi cha Vijana Mlimani blocks kimenufaika na sehemu ya fedha hizo na kujipatia shilingi Million 36.
Fedha hizo zimewezesha uanzishwaji wa kiwanda cha uzalishaji wa matofali ikiwa ni hatua muhimu ya uanzishwaji wa viwanda vidogovidogo vitakavyochagiza ukuaji wa ajira kwa vijana na hivyo kupanua uchumi miongoni mwao na taifa Kwa ujumla.
Kikundi hicho chenye wanachama 8 awali kilikuwa na machine ya kufyatulia tofali ambayo kwa wastani ilikuwa na uwezo wa kuzalisha tofali 500 kwa siku.
George Matemu ndiye kiongozi wa kikundi hicho, na anaishukuru Halmashauri kwa kuwakopesha kiasi hicho cha fedha kwani kwa sasa wamenunua mashine yenye uwezo wa kufyatua tofari 2000 mpaka 3000 kwa siku.
Mpaka sasa baada ya kupata mashine mpya kiwanda kinauwezo wa kuuza tofari kwa wastani wa 1000-2000 kwa siku kulingana na mahitaji.Bwana Matemu anaongeza kuwa kwa sasa wamepanua ajira kwa vijana kwa kuajiri vijana watano kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na mpango ni kufikia mpaka ajira ya vijana 10 kwa kuanzia wakilenga makundi ya yatima na vijana wanaozurura mtaani."Hii itapunguza uzururaji kwa vijana na hivyo kujipatia kipato halali hatimaye kuboresha maisha yao na familia zao kwa ujumla" Ameongeza bwana Matemu.
MNYORORO WA AJIRA WAPANUKA
Ayub Mwandenuka ni mnufaika wa kikundi kwa kupata ajira ambapo kila baada ya siku mbili hulipwa ujira wake.Mwandenuka anashuhudia kuwa tangu ajiunge na kikundi hicho ameweza kuihudumia familia yake, kutoa michango mbalimbali katika shughuli za kijamii na yeye kutoa ajira kwa kijana anayekata majani ya mifugo ambapo humlipa shilingi 2000 kwa siku huku akipeleka maziwa katika kituo cha mauzo ambako pia maziwa yake yameongeza ajira kwa mkusanya maziwa ambaye kila mfugaji hutoa shilingi 500 kwa siku kama ujira wake.Huu ni mchango mkubwa wa kiwanda hiki kupanua ajira mpaka kufikia sekta zingine kuongeza uzalishaji.
ONGEZEKO LA MIRADI YA UJENZI
Kufuatia Serikali Kumwaga Mabilion ya Shilingi katika Wilaya Rungwe mahitaji ya matofali kwa ajili ya shughuli ya ujenzi ni muhimu sana.Matofali yanayozalishwa katika maeneo mbalimbali ni kidogo kiasi cha kutoweza kukidhi ujenzi wa miradi hiyo.
Uwepo wa kiwanda hiki kunaenda kutatua changamoto na uharakishaji miradi ya ujenzi.Mathalani Hospitali ya wilaya Tukuyu (Makandana) imepatiwa shilingi Billion moja kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya na ukarabati wa majengo mengine
.Serikali imemwaga shilingi Million 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Msasani. Pia shillingi miilion 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha afya kata ya Iponjola.Uwepo wa kikundi hiki utasaidia upatikanaji wa tofali kwa wakati na hivyo kukuza mtaji wa kikundi, kujerejesha marejesho kwa wakati na hivyo kuwa na nafasi nzuri ya kupatiwa mkopo mwingine siku za usoni.
KIKUNDI HIKI KINAPATINANA WAPI?
Kikundi cha Mlimani Blocks Kipo kando ya barabara ya Tukuyu- kyela Mita chache kutoka shule ya sekondari Tukuyu karibu na Kivanga Garden.
MKURUGENZI ATOA NENO KWA VIKUNDI
Katika hafla fupi ya utoaji wa mikopo kwa vikundi 17 hapo jana Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Rungwe bwana Renatus Mchau alionya vikundi kuto gawana fedha walizokopeshwa kwani kufanya hivyo wanaenda kinyume na sera ya utoaji mikopo kwa vikundi, kushindwa kuinua uchumi wa pamoja, na hatimaye kutokuwa na uwezo wa kurudisha marejesho kwa wakati.
KUKUNDI KINGINE CHANUFAIKA NA MKOPO WA KIWANDA
Kikundi cha Bamboo group kilichopo katika kata ya Isongole (Namba one) kimenufaika na mkopo wa shilingi million 50 kwa ajili ya uendelezaji wa kiwanda kinachochakata bidhaa za mianzi ikiwemo utengenezaji wa vijiti vya kuchokonolea meno, Samani za ndani ya nyumba, celling board, na nyingine nyingi.
KUONA VIKUNDI VINGINE VILIVYO NUFAIKA NA MKOPO HUU BONYEZA KIUNGANISHI HIKI: https://www.rungwedc.go.tz/.../vikundi-vya-wanawake...
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa