RUNGWE NI CHAGUO LAKO HAKIKA.
Kutoka katikati ya mji wa Tukuyu tunakusogezea fursa lukuki za Uwekezaji.
Takribani km 16 kwa kila upande wa dira ya dunia unakutana na vivutio vya utalii vinavyokupa nafasi ya kuifanya siku yako ianze na kuisha vizuri.
Ukiwa hapa unauona mbele tu ya ncha ya macho yako Mlima mrefu kuliko yote nyanda za juu Kusini na wa tatu kwa urefu Tanzania (Mlima RUNGWE- www.tfs.go.tz)
Ziwa Kisiba, Maporomoko ya maji Malamba, Kaporogwe, Malasusa Kapiki, Isabula, Mwandambo, ziwa Ndwati, Ngosi, Isongole fishing camp, Kijungu, daraja la Mungu na hifadhi ya misitu na makumbusho ya RUNGWE- mission .
Maeneo haya yanafaa kwa ajili ya uwekezaji katika malazi, chakula, michezo na upigaji picha na yote yanafikikika mwaka mzima.
Rungwe inakupa nafasi ya kuwekeza katika sekta ya Viwanda hususani usindikaji wa mazao ya ndizi, kahawa, chai, Kakao, viazi mviringo, parachichi, nanasi , mazao ya misitu na Maziwa. Tembelea tovuti yetu www.rungwedc.go.tz kuona fursa na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.
https://rungwedc.go.tz/economic-activity/mpango-mkakati-halmashauri-ya-wilaya-ya-rungwe-sp-20212022
Uwepo wa chemichemi za maji za kutosha kila pembe ya wilaya inakufungulia fursa ya kujenga viwanda vya maji na tayari viwanda viwili vinaendelea na uzalishaji maji ya chupa ya kunywa.
Aidha ukiwa kando ya mnara huu kuna ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ambapo utapata msaada wa kitaalamu kwa ukaribu zaidi
Ofisi ya Rais - Tamisemi Ikulu Mawasiliano Msemaji Mkuu wa Serikali
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa