Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dkt Vicent Anney ameikabidhi kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya jumla ya vyumba 55 vya madarasa pamoja na viti na meza 2750 vilivyotarajia kugharimu jumla ya shilingi Billion 1.1 huku million 24 zikisalia ikiwa ni baki ya gharama hiyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera (Mwenye suti nyeusi) ameishukuru Baraza la madiwani,Menejimenti, watumishi pamoja na wakazi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kusimamia na kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kuagiza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu Januari 2022 wapatao 6078 kufanya hivyo mapema kutokana na kuwa na madarasa mazuri ya kusomea na kujifunzia huku kila mwanafunzi akiwa na kiti chake pamoja na meza.Pamoja na shule za sekondari 37 zilizopo, Halmashauri imejenga shule zingine mpya 5 zinazotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni. Shule hizo ni Igogwe, Kikota, Kibisi, Isaka na Kyobo
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa