· Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera leo mapema tarehe 14.6.2021 amekutana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ambapo ameagiza kila mtumishi kufanya kazi Kwa bidii huku akiongeza ubunifu wenye kuleta tija na manufaa Kwa wananchi.
Aidha ameipongeza Halmashauri Kwa kukusanya MAPATO Kwa ufanisi mkubwa hadi kufikia asilimia 93% hali itakayochochea Maendeleo Kwa mwananchi mmojammoja na taifa Kwa ujumla .
" Menejimenti na watumishi wote mmefanya kazi kubwa ya kukusanya mapato, hongera Sana! Niwaagize sasa watendaji wa kata kuleta marejesho Kwa wakati kwa kuwa hizi ni fedha za umma"
"Naamini asilimia Saba iliyobaki inaweza kumalizika haraka iwapo ukusanyaji wa MAPATO ukifanyika Kwa bidii Kwa siku chache zilizobaki kufunga mwaka huu wa fedha"
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bi. Angelina Lutambi (Kwenye skafu katikakati) ameomba watumishi wote kutoa huduma bora Kwa wananchi, kuzingatia uadilifu kazini, kutenda haki ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mazuri kazini.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Julius Chalya amesema kuwa watumishi wameendea kufanya kazi Kwa bidii huku miradi kadhaa ikitekelezwa akiutaja mradi mkubwa kupanua Chanzo cha maji Ikama ( MTO Mbaka) ambao utaharakisha usambazaji wa maji katika Mji wa Tukuyu ambapo katika hatua za awali jumla ya shilingi Million 500 zinatarajiwa kutumika.
Awali Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi. Loema Peter amesema kuwa Rungwe ina jumla ya watumishi wenye ajira ya kudumu wapatao 3226 na vibarua 82 na serikali imeendelea kulipa madai ya watumishi mbalimbali pamoja na promosheni ikiwa ni hatua ya kuongeza ari na ufanisi kazini.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa