Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amefanya ziara katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe huku akitembelea miradi kadhaa ukiwemo mradi mkubwa wa ukarabati na ujenzi wa shule ya sekondari Rungwe, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Isyonje, Salemu, Goje pamoja na kituo cha Afya Mpuguso.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ndanto Mhe.Chalamila amewaomba wakazi wa kata hiyo kuendelea kutunza amani kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kuwakwamua katika migogoro ambayo matokeo yake huchochea umasikini na kuficha utajiri walio nao wa ardhi yenye rutuba ambayo mpaka sasa imewapandisha katika mnara wa kuwa wazalishaji wakubwa na bora katika zao la viazi mviringo pamoja na mahindi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter amewaomba wakazi hao kuendelea kushirikiana na wenyeviti wa vijiji vyao katika kujiletea maendeleo badala ya kuendekeza siasa hali inayosababisha kushindwa kujitatulia changamoto za maisha yao.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Julius Chalya amewaomba wakazi wa wilaya hiyo kuendelea kutunza miradi hiyo kwani imetumia fedha nyingi za walipa kodi na serikali itahakikisha inadumu kwa kizazi hiki na kijacho
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa