Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe akishirikiana na wataalamu wake wameandaa Rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2019/2020 na kufanya majadiliano katika kikao cha menejimenti kilicho fanyika tarehe 15/01/2019 katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri. Katika kikao hicho walijadili rasimu hiyo kwa kuzingatia Mapato ya ndani, Viwanda, Uwekezaji, Elimu ,Afya na maji.
Kikao hicho kilichofanyika ni maandalizi ya vikao vya bajeti ambavyo kamati mbalimbali hukaa na kujadili Rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020. Kamati hizo ni Kamati ya ukaguzi,Kamati ya elimu afya na maji, kamati ya huduma za kijamii, kamati ya ushauri ya Wilaya(DCC), kamati ya fedha,uongozi na mipango, Baraza la wafanyakazi na Baraza la Madiwani.
(pichani ni baadhi ya wakuu wa idara wakiwa katika kikao .....picha zote na Suzan Mhoja)
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa