Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo tarehe 13.1.2022 limepitisha kwa kauli moja rasimu ya Bajeti ya Shilingi Billion 48,901,485,555.00 kwa mwaka wa fedha 2022/23 huku makusanyo kutokana na vyanzo vya ndani yakipanda mpaka kufikia shilingi Billion 6,131,460,258.00 mbele ya makusanyo ya msimu uliopita ya shilingi Billion 5,306,258756.00 ikiwa ni ongezeko la shilingi 799,885495.00 sawa na asilimia 15.07%Makusanyo ya ndani yameongezeka kutokana makisio kwenye vyanzo vifuatavyo, Ada za huduma za afya, ada za shule na michango, Adhabu za ukiukwaji sheria ndogo za Halmashauri, Ushuru wa huduma na ushuru wa mazao ya kilimo.
Bajeti hii itaenda kuinua na kuboresha miundombinu ya Biashara na masoko pamoja na ukusanyaji wa mapato, Kuboresha miundombinu ya elimu na afya, Kuboresha miundombinu ya uwekezaji pamoja na kuendeleza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ili kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla na kuboresha mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watumishi.Awali akiwasilisha rasimu hii Kaimu Afisa Mipango Wilaya Bwana Shujaa Hassan ameeleza kuwa mpaka kufikia Disemba 2021 Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 27,484,471,936.84 sawa na asilimia 52.22% ya makisio yote.
Makusanyo hayo yamesaidia kufanikisha mambo yafuatayo:
1.ujenzi wa kituo cha afya kinyala
2.Ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Ilima, Lyebe, kinyika, na Sekondari ya Masukulu pamoja na Kibisi/Kyimo
3.Kuanzisha kitalu cha miche ya miti ya kisasa na uboreshaji wa kivutio cha Ziwa kisiba/Masoko
4. Ujenzi wa kituo cha afya kata ya Ndanto na ukamilishaji wa vyumba madarasa katika shule ya sekondari Kalengo, Itagata, na Ndembela one
5.Halmashauri imebadilisha vyeo (recategorization) watumishi 1306.
6.Halmashauri imetoa mkopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu wenye thamani ya shilingi 251,000,000,.00
7. Halmashauri imefanikiwa kuondoa mrundikano wa taka mjini na baadhi ya vijiji/ vitongoji
8. Kupunguza vifo vya mama na mtoto kutoka vifo 10 mwaka 2019 mpaka kufikia vifo 6 Disemba mwaka 2021
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa