Mbele ya Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani Leo tarehe 19.01.2023, Kaimu Afisa Mipango Wilaya ya Rungwe Bwana Noah Sikwese amewasilisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Rungwe- Mwankenja.
Bwana Sikwese ameeleza kuwa Halmashauri katika mwaka wa fedha 2023/24 inatarajia kukusanya na kutumia kiasi Cha shilingi Billion 58,197,398,459.00 huku jicho likiangazia kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa shilingi Billion 11.4, Mishahara billion 40.2 na Matumizi ya Kawaida billion 6.5
Halmashauri inategemea kukusanya mapato yake kutoka Serikali kuu, Mapato ya ndani na Wahisani.
Kwa kutumia Rasimu ya Bajeti hiyo, Halmashauri inatarajia kutekeleza miradi ya Maendeleo kama ukamilishaji na ujenzi wa miradi ya afya ,elimu, na Utawala, ununuzi wa magari mawili ya upakiaji taka, Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, upanuzi wa sekta ya kilimo na Mifugo, uboreshaji wa sekta ya misitu nakadhalika.
Aidha Bwana Sikwese ameeleza kuwa
katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ilipanga kukusanya na kutumia kiasi Cha shilingi Billion 57.8 na mpaka kufikia disemba 2022 Halmashauri ilipokea kiasi Cha shilingi Billion 25.8 sawa na asilimia 44.5 huku Halmashauri kwa kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani ikikusanya shilingi Billion 3 sawa na asilimia 50.45
Hata hivyo Halmashauri ilitumia kiasi Cha shilingi Billion 23.7 sawa na asilimia 92.1 ya Fedha zilizopokekewa.
Fedha hizi zimesaidia katika ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa, Ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya Sekondari Kisondela, kupima vipande 16,650 vya ardhi na utoaji wa hati 46 mjini na hati za kimila 92. Halmashauri imefanikiwa kuanzisha kampuni tanzu ambayo itaongeza mapato ya ndani ya Halmashauri. Pia Halmashauri imefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi name yenye thamani ya shilingi 132,000,000.00
Katika hatua nyingine Bwana Sikwese ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri ilipanga kukusanya na kutumia shilingi Billion 55,192,496,716.65 na kufikia Juni 2022 ilikuwa imekusanya shilingi Billion 54, 463,545,865.1 ambapo bajeti hiyo ilitekelezwa kwa asilimia 98% na Halmshauri ikikusanya mapato yake ya ndani kwa asilimia 104%.
Baadhi ya mafanikio ya Bajeti hiyo hiyo ni ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Dharura katika Hospitali ya Wilaya Tukuyu, ujenzi wa vyumba 55 vya madarasa kwa Mpango wa UVIKO 19, Ujenzi wa jengo la ghorofa moja (OPD) Hospitali ya Wilaya Tukuyu- Makandana, ukamilishaji wa zahanati ya Ilenge na Isyonje, Ujenzi wa kituo Cha afya Ndanto, Iponjola, Kinyala na Kyimo, Ujenzi wa Bweni shule ya Msingi Katumba II, Uwekaji wa anuani za makazi maeneo yote ndani ya Halmashauri, Jumla ya watumishi 348 wamepandishwa vyeo, 131 kubadilishwa vyeo na watumishi 33 wamepata ajira mpya.
Aidha bajeti hiyo imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi 732,027,500.00 kwa vikundi 69.
Ufaulu kwa kidato Cha sita umeongezeka kutoka asilimia 99.62 mwaka 2000 Hadi asilimia 99.82 mwaka 2022.
Chanjo ya Uviko 19 kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilifanikiwa kwa ufanisi mkubwa kwa asilimia 99%
Rasimu ya Bajeti 2023/24 inapatikana kupitia www.rungwedc.go.tz
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa