Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto chini ya miaka ( 8) imezinduliwa leo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
Programu hii inatekelezwa kwa muda wa miaka mitano 2021/22-2025/26
Mpango huu umelenga kutatua changamoto za ukuaji na maendeleo ya ya watoto walio na umri wa miaka 0-8
Programu itahakikisha inatoa mchango katika kufanikisha Mpango wa taifa wa Maendeleo wa miaka mitano 2021/22-2025/26 na hivyo kusaidia kulifikisha taifa katika uchumi wa kati.
Programu imejikita katika mambo matano katika kuhakikisha dira ya taifa inafikiwa ipasavyo.
LISHE: Kuhakikisha watoto wanapata chakula chenye viini lishe na hivyo kuwajengea afya bora ya akili sambamba na kuwaepusha na Udumavu pamoja na Utapiamlo.
MALEZI YENYE MWITIKIO: Kuhakikisha mtoto anapata malezi bora na mzazi kuitikia hisia za mtoto mara kwa mara na hivyo kutoa msaada wa karibu kwa ufanisi mkubwa.
ELIMU YA AWALI: Kuhakikisha mtoto anapata elimu ya awali na kupewa stadi muhimu kwa ajili ya makuzi ya mtoto pamoja na michezo mbalimbali ili kumjengea uchangamshi na hivyo kuboresha ubongo na misuli ya mtoto.
ULINZI: Kuhakikisha mtoto anapata ulinzi wa kutosha dhidi ya vitendo vya ukatili wa kisaikolojia na kimwili. Vitendo vingine kama ubakaji, ulawiti, matusi, adhabu, kutopewa chakula, na usalama wa mtoto akiwa barabarani, na dhidi ya wanyama wakali.
AFYA: Kuhakikisha mtoto anapata matibabu mara kwa mara ikiwemo chanjo na vipimo mbalimbali vya afya ya mwili na hivyo kumjengea mtoto uimara na utimamu wa mwili.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa