Jumla ya pikipiki NNE zimetolewa Kwa watendaji wa kata NNE katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe ikiwa ni sehemu ya motisha na chachu ya utawala bora pamoja na ukusanyaji wa MAPATO.
Akikabidhi pikipiki hizo Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bi. Loema peter ( mwenye nguo nyekundu) amewaomba watendaji wa Kata zingine kufanya kazi Kwa bidii Kwa lengo la kuinua pato la halmashauri ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma bora Kwa wananchi.
"Zoezi la utoaji wa nyenzo hizi za kazi ni endelevu hivyo kila Mtendaji lazima ahakikishe anafikia kilele stahiki cha mafanikio" Amesisitiza.
Kata zilizopata tuzo za pikipiki, vyeti pamoja na fedha taslimu ni pamoja na kata ya Ikuti Makandana, Itagata na Mpuguso.
PICHA JUU: Mweka hazina wilaya bwana Lucas Ndobele akijaribu pikipiki kabla ya kuzikabidhi Kwa watendaji wa kata mapema Leo
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa