Wakazi wa kata ya Mpuguso wameunganisha nguvu na kujenga bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Mpuguso kwa zaidi ya zaidi ya shilingi Miliion 32 ikiwa ni Michango ya Wananchi ambapo hatua hii itasaidia kupanua upatikanaji wa elimu bora, kupunguza wanafunzi kutembea umbali mrefu zaidi ya KM 7 kutoka vijiji vya Isajilo, Mpumbuli na maeneo mengine.
Hii ndiyo faida ya Ushirikishwaji wa wananchi katika kuibua na kutekeleza miradi sambamba na Mpango wa Fursa na Vikwazo (O&D) katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ambapo serikali imekuwa ikiwaunga wananchi mkono katika hatua mbalimbali.
Bweni kama hili limejengwa na wananchi wa kata ya kiwira katika shule ya sekondari kiwira ambapo lipo katika hatua ya Ukamilishaji, Zahanati ya Ishinga na Isebero na kituo cha afya kata ya Swaya , Ujenzi wa shule za Msingi Sanswago, Chief Mwanjali, Halanzi na miradi mingine mingi
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa